Sahau changamoto za kutunza rekodi kwa makaratasi. Kikoba Janja hurahisisha usimamizi wa michango, mikopo, na taarifa za wanachama kwa uwazi na usalama.
Kiongozi anasajili kikundi na kuweka sheria za msingi kama vile riba ya mikopo na adhabu.
Baada ya usajili, kiongozi anaweza kuongeza wanachama wote kwenye mfumo na kuwapa akaunti zao.
Rekodi michango, toa mikopo, na fuatilia marejesho kwa urahisi. Kila mwanachama anaona taarifa zake.
Kila mwanachama anaona taarifa zake binafsi kwa wakati wowote, na viongozi pekee ndio wenye ruhusa ya kuhariri rekodi. Hii inajenga kuaminiana.
Viongozi hawatumii tena muda mwingi kwenye mahesabu ya riba, adhabu, na kufuatilia madeni. Mfumo hufanya kazi hizi kiurahisi na kwa haraka.
Pata ripoti za kifedha za kikundi na za mwanachama mmoja mmoja kwa kubofya kitufe. Hii inasaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.